logo

logo
...

Tuesday, May 26, 2015

IMANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI                                                                                                                

Binadamu wote ni sawa, kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyamavya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).


HABARI MPYA


ZIARA YA KINANA WILAYA YA CHEMBA YAFANA SANA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulraman Kinana akihutubia wakazi wa Itolwa wilayani Chemba mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara zake za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010.
read more

TUESDAY, NOVEMBER 25, 2014


KINANA ATINGA MASASI, ATAKA CCM IENDELEE KUIBANA SERIKALI JUU YA WAFUJAJI WA FEDHA ZA UMMA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi na kuwaambia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi alisema lazima tutangulize utumishi kwa umma.
 Kadi zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama cha NLD Taifa Ndugu Frank Rashid Maulano aliyejiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi.
Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
 Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Marika wilayani Masasi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Marika ikiwa sehemu ya kujenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi ambapo alikagua maendeleo ya mradi wa maji wa Chiungutwa mradi ambao utasaidia vijiji 27,tarafa 3 ambapo watu zaidi ya elfu 60 watanufaika na mradi huo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa wilaya ya Masasi ambapo aliwapongeza kwa kutambua utapeli wa vyama vya upinzani katika kijiji chao na kuamua kujitenga nao kabisa.

FRIDAY, OCTOBER 31, 2014


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa furaha matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Msumbiji tarehe 15 Oktoba 2014. Chama Cha Mapinduzi kilikuwa kinafuatilia kwa karibu mchakato wote wa Uchaguzi huo hasa kwa sababu Tanzania na Msumbiji ni nchi zenye uhusiano wa damu.
Kilifuatilia kwa karibu kwa kuwa pia CCM na Chama cha FRELIMO ni vyama ndugu vyenye historia moja na ya pamoja ya Ukombozi Kusini mwa Afrika.
Historia hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Mteule wa nchi hiyo Ndugu Filipe NYUSI mara baada ya kuteuliwa kwake na FRELIMO kugombea Urais, nchi ya kwanza kuitembelea kuwa Tanzania.
Ikumbukwe kwamba huyu si mgeni hapa Tanzania. Kama wanaharakati wengine wa ukombozi, Ndugu NYUSI aliishi Tanzania, anaongea vizuri Kiswahili na anaichukulia Tanzania ni nyumbani.
Kwa mnasaba huo, Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa ujumla tuna kila sababu ya kushangilia ushindi walioupata ndugu zetu wa FRELIMO, kwani ushindi wao ni ushindi wetu.
Tunampongeza sana Rais Mteule Filipe NYUSI kwa kupeperusha vema bendera ya FRELIMO. Matokeo ya Uchaguzi yamedhihirisha imani kubwa waliyonayo wana-Msumbiji kwa FRELIMO na kwa Rais Mteule Filipe NYUSI.
Tuna imani kwamba chini ya uongozi imara wa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Rais Mteule Filipe NYUSI, uhusiano kati ya vyama vyetu viwili utaimarika na kustawi.
Tunampongeza pia Rais Armando GUEBUZA kwa kuiongoza FRELIMO na Taifa lake vema na kukamilisha uongozi wake kwa mafanikio makubwa. Tunamtakia maisha tulivu ya kiongozi huyo mstaafu.
Anapoanza kipindi hiki cha uongozi wa Taifa lake, sisi wana-CCM tunamtakia Ndugu NYUSI afya njema, busara, maarifa na uongozi uliotukuka.
CCM itasimama pamoja na FRELIMO katika kuendeleza urithi ulioachwa na waasisi wa vyama vyetu Mwalimu Julius NYERERE na Ndugu Samora MACHEL.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
31/10/2014